Chelsea na Leeds United Wafikia Makubaliano ya Uhamisho wa Raphinha-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest

Chelsea na Leeds United Wafikia Makubaliano ya Uhamisho wa Raphinha-Michezoni leo

Raphinha Dias anakaribia kujiunga na klabu ya Chelsea

KLABU ya Chelsea ya nchini Uingereza pamoja na Leeds United zimefikia makubaliano rasmi ya uhamisho wa winga wa Leeds United na timu ya Taifa ya Brazil Raphinha Dias Belloli kwa ada ya kati ya paundi milioni 60-65.

 

Inaelezwa kwamba mazungumzo yanaendelea kwa sasa juu ya maslahi binafsi kati ya mchezaji pamoja na wakala wake ambaye ni kiungo wa zamani wa Chelsea raia wa Ureno Deco De Souza.

Raphinha akiwa katika uzi wa Timu ya Taifa ya Brazil

Raphinha (25) alikuwa akigombewa na vilabu vinne vya Totenham Hotspurs, Arsenal, FC Barcelona pamoja na Chelsea lakini ni Chelsea ndiyo wanaonekana kushinda na kuinasa saini ya winga huyo Mbrazil aliyekuwa na msimu mzuri akiwa na Leeds United msimu uliopita.

Raphinha ataungana na raia mwenzake wa Brazil Thiago Silva katika kikosi cha Chelsea

Kutokana na uhamisho huo Raphinha atakuwa na uhakika wa kucheza kwenye klabu ambayo inashiriki mashindano ya klabu Bingwa Barani Ulaya mara kwa mara na ataungana na Mbrazil mwenzie Thiago Silva huku Neymar Da Silva Junior naye akihusishwa na dili la kutua darajani.

 

 

 

 

The post Chelsea na Leeds United Wafikia Makubaliano ya Uhamisho wa Raphinha appeared first on Global Publishers.





Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz