BAO pekee la mshambuliaji wa Lyon ya Ufaransa, Karl Louis-Brillant Toko-Ekambi dakika ya 30, limewapa Cameroon ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Burundi katika mchezo wa Kundi C kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika jana Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Kwa matokeo hayo, Simba Wasiofungika wanapanda kileleni baada ya kubeba pointi hizo tatu katika mechi yao ya kwanza, wakati Burundi inabaki na pointi yake moja kufuatia sare ya 1-1 ugenini na Namibia kwenye mechi ya kwanza.

Timu nyingine kwenye kundi hilo, Kenya imeondolewa kutokana na kufungiwa na FIFA.
No comments:
Post a Comment