Saa kadhaa baada ya Simba SC Kuthibitisha kuachana na Kocha Pablo Franco kwa Makubaliano ya kuvunja Mkataba, imefahamika kuwa Kocha huyo alikua na ofa nono mkononi mwake.
Klabu ya Amazulu inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini ilimtumia ofa Kocha Panlo tangu Mei 20 mwaka huu na kumtaka athibitishe kukubali ama kukataa ndani ya siku kumi yaani hadi Mei 30.
Barua ya Amazulu kwenda kwa Kocha Pablo imevuja na Kusambaa katika mitandao ya kijamii, ambapo inaonyesha sehemu ya ofa aliyotumiwa akiwa bado Mkuu wa Benchi la Ufundi Simba SC.
Amazulu imesisitiza kumlipa Mshahara wa Randi 525,000 (sawa na zaidi ya Shilingi Milioni 77 za Tanzania), Nyumba kwa ajili ya makazi, Gari ya kutembelea pamoja na Kadi ya kujaza mafuta kila mwezi, Tiketi mbili za Ndege Daraja la Kwanza kwa kila msimu (Kwenda na Kurudi nyumbani kwao Hispania).
Huenda maamuzi ya kuachana na Simba SC leo Jumanne (Mei 31), yakawa na faida kwa Kocha Pablo ambaye pia inadaiwa anawindwa na klabu ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini na Raja Casablanca ya Morocco.
No comments:
Post a Comment