Zari Hassan The Boss Lady Mama Watoto wa Diamond Platnumz Atua Bongo - EDUSPORTSTZ

Latest

Zari Hassan The Boss Lady Mama Watoto wa Diamond Platnumz Atua Bongo



Mfanyabiashara na Msanii maarufu kutokea Uganda mwenye makazi yake nchini Afrika Kusini, @ZariTheBosslady ametua Tanzania kwa zoezi la kurejesha kwa jamii kuelekea siku ya hedhi salama duniani Mei 28 mwaka huu.


Zari yuko Tanzania ambapo katika sehemu ya zoezi hilo mapema leo Mei 14 2022 ametoa taulo za kike kwa shule za msingi na sekondari kwa wanafunzi wa kike kuelekea siku hiyo inayoadhimishwa kila mwaka duniani.


Zari kama balozi wa Dowecare akishirikiana na kampuni hiyo wametoa msaada huo wa taulo za kike kwa shule za Msingi na Sekondari za wilaya ya Misungwi.





Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz