Nape Akaribisha Canada Kujenga Viwanda vya Simu za Smart Phone Hapa Tanzania - EDUSPORTSTZ

Latest

Nape Akaribisha Canada Kujenga Viwanda vya Simu za Smart Phone Hapa TanzaniaWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amewakaribisha wawekezaji kutoka Canada kuja kuwekeza katika viwanda vya utengenezaji wa simu janja hapa nchini.

Nape amesema hayo katika kikao cha kubadilishana uzoefu na Katibu wa Mambo ya Nje wa Canada, Robert Oliphant ambapo walijadili masuala mbalimbali ya habari na teknolojia ya habari, leo Mei 26, 2022 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.

"Eneo ambalo tulitamani kama serikali kupata wawekezaji, ni eneo la upatikanaji wa simu janja (smart phones na tablets), ili ziwe bei nafuu na watu waweze kumudu kununua," alifafanua Nape.

Aliendelea kusema kuwa, kutokana na Tanzania kutokuwa na viwanda vya kutengeneza simu janja imesababisha vifaa hivyo kuwa na gharama ya juu, hivyo kupelekea idadi chache ya Watanzania kuweza kumiliki simu hizo.

Nape amesema kuwa, ni asilimia 27% tu ya Watanzania ndio wanaomiliki simu janja na asilimia inayobaki wanamiliki simu za kawaida, kutokana na gharama ya simu janja kuwa ya juu.

"Sasa imefika wakati simu janja zizalishwe hapa nchini, ili bei iwe ya chini na kila Mtanzania aweze kupata kifaa hicho, na hata huduma ikiboreshwa ina maana watu wengi watapata hiyo huduma," alifafanua Nape.

Kwa upande wake, Katibu wa Mambo ya Nje wa Canada, Robert Oliphant amesema kuwa ili Tanzania iweze kuwa na mawasiliano ya uhakika inatakiwa kuweka vipaumbele eneo la nishati, maendeleo pamoja na watu wenye ujuzi wa teknolojia ya habari na mawasiliano.


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz