Kiungo wa ASEC Mimosas Stephen Aziz Ki Ajipeleka Simba, Baada Kudaiwa Kuwaniwa na Yanga-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest

Kiungo wa ASEC Mimosas Stephen Aziz Ki Ajipeleka Simba, Baada Kudaiwa Kuwaniwa na Yanga-Michezoni leo

Stephen Aziz Ki, kiungo wa ASEC Mimosas (katikati) akifanya yake.

 

JINA la Stephen Aziz Ki, kiungo wa ASEC Mimosas, bado linatembea mitaa ya Kariakoo jijini Dar baada ya timu kongwe za hapa nchini, Simba na Yanga kuiwania saini yake.

 

Winga huyo ambaye hivi karibuni ilielezwa kwamba Yanga wanakaribia kupata saini yake kwa ajili ya msimu ujao, kwa sasa Simba wanaonekana kuwa karibu zaidi kumchukua.

 

Mchezaji huyo raia wa Burkina Faso, anasimamiwa na mfanyabiashara Idriss Diallo ambaye kwa sasa ni Rais wa Shirikisho la Soka Ivory Coast (FIF).

 

Chanzo chetu kutoka Simba, kimeliambia Spoti Xtra kuwa, baada ya uongozi wa klabu hiyo kuanza harakati za kuiwania saini ya Aziz Ki, ulirudi nyuma kutokana na RS Berkane ya Morocco kuingilia dili hilo.

 

Mtoa taarifa huyo aliendelea kueleza kwamba, kwa sasa matumaini ya kumpata yamerudi tena baada ya mchezaji mwenyewe kuonesha nia ya kujiunga na Simba, huku akiwapa mbinu za kumpata kirahisi.

 

“Ilifikia kidogo tu tukate tamaa ya kumnasa Aziz Ki, ila tunamshukuru sana yeye mwenyewe baada ya kuonesha nia ya kutaka kujiunga na sisi.

 

“Hii ni baada ya kutuambia mtu pekee anayeweza kupokea ofa yetu ni Rais wa Shirikisho la Soka Ivory Coast, Idriss Diallo anayemsimamia ambaye tayari tumemfikia.

 

“Kitendo cha mchezaji mwenyewe kuonesha nia ya kutaka kuichezea Simba, ndiyo imekuwa chachu yetu kurudi kwa kasi kuhakikisha dili hili linatimia haraka kabla ya mambo kuwa mengi,” kilisema chanzo hicho.

STORI NA MUSA MATEJA | GPL

 

The post Kiungo wa ASEC Mimosas Stephen Aziz Ki Ajipeleka Simba, Baada Kudaiwa Kuwaniwa na Yanga appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz