Harmonize Anavyowachanganya Mashabiki zake na Kauli zake - EDUSPORTSTZ

Latest

Harmonize Anavyowachanganya Mashabiki zake na Kauli zake
Taarifa iliyopo ni kwamba Harmonize a.k.a konde boy anawayumbisha mashabiki zake ndani ya muda mfupi sana.

Utata ulianzia hapa:-
1. kipindi Harmonize alipokwenda Marekani mwezi wa 9 mpaka mwezi wa 11 mwaka 2021, alitoa taarifa ya kutaka kuachia album yake ambayo ingeitwa Alzona baada ya kutoka huko, lakini mpaka leo hakuna hiyo album.

2. Akiwa hukohuko Los Angeles, California mwezi wa 11 tarehe Moja alitoa taarifa ya kuachia album ya High School tarehe 5 mwezi huo huo na akafanya hivyo.

3. Album ya High School ambayo ndani yake aliachia video ya nyimbo baadhi kama Teacher, Mtaje na Sandakalawe, Baada ya hizo chache kati ya nyimbo 20 kwenye Album yake, ukimya ulitanda kidogo.

4. Akaja kuutandua miezi michache iliyopita baada ya kuachia wimbo ambao hauko kwenye album ya High School, na akaunganisha na video kabisa hapa nazungumzia wimbo wa "Mwaka wangu"🤦‍♀️

5. Akafuatia nyimbo zingine tu baadae akarudi tena akasema anataka kuachia tena nyimbo za kwenye album yake ya High School.

4. Akaachia video ya Mdomo mashabiki wakaipokea tena ni juzi juzi tu lakini sasa ametutoa tena kwenye reli anataka kuachia Album nyingine ya Smoker Vision mwezi wa 6 mwaka huu.

Sasa swali ni kwamba Album ya Alzona ilibadilishwa jina na kuwa High School? au ni Harmonize anafanya mziki kwa mzuka, bila mpangilio, au labda uongozi wake unashindwa kumaliza wanayoyaanzisha kwa harmonize?

Sio ushabiki ila ni hoja tu kwasababu mashabiki wanadundadunda kama kitenesi yaani🤦‍♀️

NB: Mashabiki zako wanakupenda sana Konde, kuna pahala kidogo tu unakosea, rekebisha kaka alafu tupe vitu roho inapenda😉

Na @deedy_diana

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz