Alikamwe "Mambo 10 nilioyaona YANGA vs SIMBA" - EDUSPORTSTZ

Latest

Alikamwe "Mambo 10 nilioyaona YANGA vs SIMBA"1: MWANZA IS GREEN & YELLOW🟢🟡 WASIOAMINI WAMEAMINI KWA MACHO YAO.. YANGA WAMESTAHILI KWENDA FAINALI✊

2: PROFESA NABI🙌 SIMPLY, ANASTAHILI KUWA MAN OF THE MATCH 👏 Alimuweka PABLO kwenye kiganja chake na kumpa maswali magumu sana kiwanjani. Mechi Iliisha kwenye Mkoba wake wa mbinu

3: Dakika 180 za Ligi, Nabi alikwenda na mfumo wa 4-2-3-1 Lakini hapa MWANZA AKAJA NA 3-5-2! Approach ikiwa ni kushambulia kwenye kipindi cha kwanza. Hatua za Djuma na Shomari zikileta vurugu kubwa kwa mistari miwili ya ulinzi ya Simba.. Kivipi?

4: Kumbuka Yanga walianza na 'Dabo Straika'! Hapa Henock na Onyango wakawa 'bize' uwanjani. Ile 'Battle' ya 3v3 katikati ya kiwanja ikawa inaamuliwa na 'Movements' za 'Wing back' za Yanga. Taddeo Lwanga akapata mechi ngumu zaidi ya 'Derby' tangu atue Tanzania

5: Bila 'Key Players' wake baadhi, Sielewi kwanini PABLO aliamua kuanza mechi ya 4-3-3 akiwa na mpango wa kushambulia. Kanoute na Muzamir 'No creativity' miguuni mwao ndio Pablo aliwapanga kama Offensive wawili wa juu. Hapa Simba ilijikaba yenyewe

6: FEISAL SALUM.. BAO LA ROYAL TOUR✊ WHAT A HIT.. Unaelewa kwanini kipindi cha pili, Nabi alimpumzisha. Kipindi cha kwanza alikimbia eneo kubwa sana, kulia na kushoto katikati ya mistari miwili ya ulinzi.. What A Perfomance

7: SURE BOY. SURE BOY. SURE BOY. UKIUPENDA MPIRA, UTAMPENDA SURE BOY! Inatosha sana kusema hivyo.

8: Mugalu nafiriki dakika 90 za leo amewapa pakuanzia viongozi wa Simba kuelekea dirisha la usajili. Alicheza kwa presha, Utulivu mdogo.. Ni kama alikamia sana mechi kiasi cha kumpotezea umakini wake uwanjani.. Na Kama REFA ARAJIGA ANGEKUA MKATILI, Pengine Mugalu angeweza kupata Red Card

9: Well Done Shabani Djuma 🙌 Well Done DIARRA! Hatari pekee ya Simba uwanjani ilikuwa kwenye mipira ya juu na kwa asilimia 85, Diarra alikuwa bora sana kwenye eneo hilo

10: Henock anabaki na heshima yake ya Derby. Simba imepoteza Lakini kila shabiki wa Yanga ataondoka uwanjani akikiri Ubora wa Henock.. 👏

Nb: Walichobakiza ni kugombea MO COLA😃
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz