NBC Yazidi Kuinogesha Ligi Kuu, Yatoa Tuzo/Fedha Kwa Mchezaji Bora wa Mwezi-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest

NBC Yazidi Kuinogesha Ligi Kuu, Yatoa Tuzo/Fedha Kwa Mchezaji Bora wa Mwezi-Michezoni leo

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesema itaendelea kuboresha masuala mbalimbali ya kimichezo sambamba na kutoa hamasa kwa wachezaji.
NBC kama mdhamini wa Ligi Kuu Tanzania bara imetoa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Desemba Reliant Lusajo na kumpatia mfano wa hundi ya Shiling milion moja.
Akizungumza na waandishi, Mkuu wa Chapa na Mawasiliano David Raymond alisema NBC itaendeea kutoa hamasa kwa wachezaji na makocha kwa kil mwezi ili kukuza soko la ndani.
Alisema, katika kukuza soka la kiushindani kwa wachezaji wa ndani wamedhamiria kuboresha hali za wachezaji kwa kuwapatia zawadi za kila mwezi pamoja na kocha bora.
“Tumedhamiria kuboresha soko la ndani la wachezaji, na makocha kwa kuwapatia tuzo za kila mwezi ili kuhamasisha wafanye vizuri na kujitangaza kimataifa,”amesema Raymond
“Kwa leo tumekuja kutoa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Desemba Reliant Lusajo na tunarajia kutoa kwa Clatous Chama kwenye mechi ya Derby,”
Akielezea kuendelea kutoa hamasa kwa wachezaji, Raymond alisema huon ni mwanzo wataendelea kuboresha tuzo mbalimbali za wachezaji na kufika mbali.

The post NBC Yazidi Kuinogesha Ligi Kuu, Yatoa Tuzo/Fedha Kwa Mchezaji Bora wa Mwezi appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz