KOCHA wa zamani wa Simba, Patrick Aussems Aipa Yanga Ushindi - EDUSPORTSTZ

Latest

KOCHA wa zamani wa Simba, Patrick Aussems Aipa Yanga UshindiKOCHA wa zamani wa Simba, Patrick Aussems, raia wa Ubelgiji, ameweka wazi kuwa kwa upande wake, anaona Yanga wana nafasi kubwa katika mchezo wa kesho Jumamosi dhidi ya Simba kutokana na kubebwa na rekodi ya matokeo ya mechi zao zilizopita, tofauti na wapinzani wao.

Aussems ambaye kwa sasa ni Kocha wa AFC Leopards ya Kenya, ametoa kauli hiyo kuelekea katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara ambao utazikutanisha Simba na Yanga.


 Akizungumza na Championi , Aussems alisema

“Nadhani kwangu naona Yanga wanayo nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo kutokana na rekodi ya mechi za mwisho kwenye ligi, tofauti na Simba ambao wametoka kupata sare halafu wameondolewa kwenye Kombe la Shirikisho Afrika. Inaonyesha kwao kukata tamaa japokuwa lolote linaweza kutokea.

GPL
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz