elru87tYGBGEm Kiungo Mrundi Amchambua Fei Toto wa Yanga, Atamani Kucheza Pamoja-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest

Kiungo Mrundi Amchambua Fei Toto wa Yanga, Atamani Kucheza Pamoja-Michezoni leo

Ismail Nshimiyimana ‘Pitchou’

KIUNGO mkabaji wa Kiyovu ya Rwanda, Mrundi, Ismail Nshimiyimana ‘Pitchou’, amefunguka kuwa, haitakuwa shida kwake kama ikitokea anapata nafasi ya kucheza sambamba na kiungo mshambuliaji wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei ToTo’ kutokana na uwezo mkubwa alionao licha ya kuheshimu uwepo wa Mganda, Khalid Aucho.

 

Pitchou ametoa kauli hiyo kufuatia wiki iliopita kufuatwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Yanga, Injinia Hersi Said, akiwa na Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze ambao walikuwa nchini Rwanda kwa ajili ya kumfuatilia kiungo huyo sambamba na pacha wake Abed Bigirimana ambao wote wanachezea Kiyovu.

Feisal Salum ‘Fei ToTo’.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Pictchou alisema kuwa amekuwa akiifuatilia timu hiyo katika mechi zake za ligi lakini amekuwa akitamani kucheza pomoja na Fei Toto kutokana na uwezo mkubwa alionao akicheza katika nafasi ya kiungo mshambuliaji kwa kuamini watafanya makubwa.

 

“Nadhani kwangu ikitokea nakuja Yanga natamani kuona napata nafasi ya kucheza na Fei kwa sababu kwanza amekuwa na ubunifu lakini anajua wakati gani wa kufanya maamuzi akiwa na mpira, nadhani italeta utofauti mkubwa kwa kuwa nitakuwa katika eneo la chini na yeye akiwa juu tutafanya mambo makubwa.

Stori: Na Ibrahim Mussa

BARBARA AFANYA UMAFIA ATUA SAUZ MAPEMA APANGUA UMAFIA, YANGA WAMNASA SRAIKER WA MABAO….

The post Kiungo Mrundi Amchambua Fei Toto wa Yanga, Atamani Kucheza Pamoja appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz