Hakuna Mkate Mgumu… Kajala Aanza Kumlegezea Harmonize, Atoa Ujumbe Mzito - EDUSPORTSTZ

Latest

Hakuna Mkate Mgumu… Kajala Aanza Kumlegezea Harmonize, Atoa Ujumbe MzitoKuna msemo maarufu mtaani hasa kwa vijana kwamba hakuna mkate mgumu mbele ya kikombe cha chai ya rangi!

Huwenda hicho ndicho kinachoonekana kwani umekuwa mchezo mrefu wa kusubiri jibu rasmi kutoka kwa mwigizaji Kajala Masanja au Mama Pau kuhusu kuhusu ombi la msanii Harmonize ‘Konde Boy Mjeshi’ la kutaka warudiane.

Kajala amekuwa akitoa jumbe mbalimbali ambazo zimekuwa zikitafsiriwa kama majibu yasiyo ya moja kwa moja kuhusiana na ombi hilo.

Kwa mfano; kupitia Insta Story yake, Kajala ameandika; “No one knows what you feel inside…”


 
Akimaanisha hakuna anayejua namna unavyojisikia ndani yako.


Msanii Harmonize ‘Konde Boy Mjeshi’.
Kufuatia ujumbe huo, baadhi ya wafuasi wa Harmonize au Harmo ambao wanapanga kuandamana kwenda kwa Kajala kumuomba amrudie Harmonize, wanasema wamevuta pumzi kidogo kwa ujumbe huo kwani huwenda mwanamama huyo ameanza kuelewa ombi la Konde Boy.

Harmonize amekuwa akitrendi baada ya kuanza kupigana juu chini ili aweze kurudiana na Kajala waliyeachana mwaka jana kutokana na ile skendo ya ‘washa taa’ ambapo jamaa huyo alidaiwa kumtaka Paula; mtoto wa Kajala.

Baadhi ya watu wanasema Harmonize anatafuta kiki, lakini wengine wanaamini siyo kiki, ila ameleweshwa kimapenzi na Kajala.

Harmonize anasema amejaribu kuukimbia ukweli wa kimapenzi kwa kwenda zake kuanzisha penzi jipya na mwanamke kutoka Australia, Briana ila bado moyo wake umekataa kusonga mbele, badala yake umebaki katika gereza la Kajala.

STORI NA SIFAEL PAUL
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz