Hatimaye ndoa ya Kanye West na Kim Kardashian imevunjika Rasmi. - EDUSPORTSTZ

Latest

Hatimaye ndoa ya Kanye West na Kim Kardashian imevunjika Rasmi.


Hatimaye ndoa ya nyota wa muziki wa Hip hop kutoka nchini Marekani Kanye West ‘Ye’ na mwanamitindo na mjasiriamali maarufu Kim Kardashian imevunjika rasmi.

Machi 2, 2022, ndio siku ambayo kesi ya talaka imekamilika huku Jaji wa mahakama ya Los Angeles ameweka wazi kuwa Kim Kardashian kwa sasa ni mwanamke asiye kwenye ndoa na kuhitimisha kwa kuliondoa jina la West kwenye ubini wa mrembo huyo.

Ndoa ya Kanye na Kim imedumu kwa kipindi cha takribani miaka 8 pekee, ambapo walifunga ndoa yao Mei 14, mwaka 2014 na wakiwa pamoja kama mke na mume wawili hao walibarikiwa kupata watoto wanne.

Watoto hao ni North mwenye umri wa miaka 8, Saint 6, Chicago 2, pamoja na Psalm mwenye umri wa miaka miwili.


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz