Harmonize Awapa Pole Waliokosekana Kwenye TUZO Akiwemo na Msanii Wake Ibrah - EDUSPORTSTZ

Latest

Harmonize Awapa Pole Waliokosekana Kwenye TUZO Akiwemo na Msanii Wake Ibrah


“Tuzo zina maana kubwa sana, naamini zinaenda ku-inspire watu wengi, kuwaongezea speed kwenye kazi nikiwemo mimi pia na kama umeliona jina langu basi ujue nitashiriki kwa asilimia 100% Kila mtu ana haki ya kusema anachojisikia kwasababu hata hizo tuzo zingine ambazo watu wanazio bora kuliko tuzo za nyumbani zinalalamikiwa siku zote! Mfano mdogo mwaka jana tumejionea tuzo za Afrima walimeweka @marioo_tz kama Best Upcoming Artist!”

“Nadhani niipongeze na kuishukuru pia serikali kwa kuangalia wanawezaje kupanua wigo wa muziki! Mama ana mwaka mmoja tu lakini unaona ni jinsi gani ambavyo anajitahidi kutatua vitu ambavyo vimekuwa kilio kwa muda mrefu, amefanyia kazi tumepata mirabaha juzi leo tuna Tuzo zimezinduliwa, unaona kabisa ni kiasi gani anawekeza muda na nguvu kuyatatua mambo ambayo yamekuwa yakipigiwa kelele kwa muda mrefu”

“Niiombe Serikali wasikate tamaa, kila kitu kina changamoto, watuvumilie pia sisi Wasanii, sisi ni binadamu pia na ninaamini serikali ipo strong haiwezi kuyumbishwa kwa maneno ya Watu! Muda mwingine tunateleza, naamini kuwa Wasanii wengi sana hatuna tuzo za kitanzania, tupo wengi tulotamani kutimiza ndoto zetu”

“Niwaombe Mashabiki wote wakatupigie kura wote tulofanikiwa kuingia, na wale ambao hawajafanikiwa kuingia poleni akiwemo Msanii wangu @ibraah_tz, huwezi kujua watu wana nominate kwa style gani, hii ni Serikali! Naipongeza sana Serikali” -Harmonize

Konde Boy @harmonize_tz amefunguka hayo kwenye Mahojiano na Waandishi wa Habari jioni ya jana baada ya kuulizwa mtazamo wake juu ya Nominations za Tuzo za TMA.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz