Chid Benz ampa sifa Fid Q "Umeonyesha Busara, Heshima, Bila Kuwa Mbinafsi Wala Kukebehi mtu" - EDUSPORTSTZ

Latest

Chid Benz ampa sifa Fid Q "Umeonyesha Busara, Heshima, Bila Kuwa Mbinafsi Wala Kukebehi mtu"

 


Rapa Chid Benz ameonyesha kufurahishwa na mwenendo wa rapa mwenzie Fareed Qubanda maarufu Fid Q  kufuatia namna alivyoweza kushughulikia na kutafuta suluhu ya sakata la uteuzi wa Steve Nyerere kama msemaji wa Shirikisho la Muziki Tanzania.


Chid Benz ameamua kuidhihirisha heshima yake kwa Fid Q kwa kitendo cha kuweza kuvumilia maneno makali na masimango kutoka kwa watu mbalimbali wakiwamo wadau pamoja wasanii wenzie.


“Farid I like the fact umeweza control na kuonyesha yaliyo ndani yako busara, heshima, bila kuwa mbinafsi wala kukebehi mtu au watu huu ndiyo ukomavu uliyo ndani yako. Haijalishi mapungufu yaliyojitokeza (KAMA YAPO) umesimama kweli G. Hatukatahi kwenye game kuna sinto fahamu nyingi za kukatisha tamaa especially now na yanazidi kujitokeza siyo point yangu ya sasa,” alisema Chid.


Chid Benz ameutumia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram kuchapisha ujumbe huo kama sehemu ya kuuthibitishia umma alichokiona kwa Fid Q katika kipindi chote cha changamoto hiyo.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz