Huyu ndiye Aliyemuoa Diva Loveness Mtangazaji wa Wasafi - EDUSPORTSTZ

Latest

Huyu ndiye Aliyemuoa Diva Loveness Mtangazaji wa Wasafi
USIKU Waopendanao duniani, Valentine’s Day 2022; muda wa saa mbili usiku, mtangazaji wa Wasafi, Diva Gissele Malinzi au Diva The Bawse alidai kufunga ndoa ya Kiislam na mwanamue aliyefahamika kwa jina la Abdul.

Mrembo huyo alitoa taarifa za ndoa yake hiyo katika kipindi chake cha Lavidavi na kudai kuwa, aliamua kufunga ndoa ya siri na kijana huyo kwa sababu ndiye mtu aliyekuwa akimtaka.

“Usiku wa Valentine, muda wa saa mbili usiku, nilifunga ndoa na mume wangu, Abdul na ndoa hiyo ilihudhuriwa na watu wasiozidi kumi, kwa sababu nilitaka iwe hivyo, lakini sasa hivi tupo kwenye maandalizi ya kufanya sherehe kubwa ya ndoa yangu,” alisema Diva.


Hata hivyo, swali la wengi limekuwa ni juu ya mwanaume huyo ni nani hasa? Katika kuchimba, Gazeti la IJUMAA limebaini kuwa, mwanaume huyo anaitwa Abdulrazak Salum na alijipatia umaarufu mkubwa mitandaoni kutokana na video zake anazojirekodi kwa ajili ya kuelimisha jamii hususan wapendanao na namna ya kuishi vizuri na mwanamke au mwanaume wako.


Inadaiwa kuwa, uhusiano wao wa kimapenzi ulianza tangu mwaka 2019. Wakiwa ndani ya mahaba mazito Septemba, 2021, Diva alimualika Abdul katika kipindi chake cha Lavidavi na kufanya naye mahojiano marefu na leo hii wawili hao wamefikia hatua ya kufunga ndoa takatifu na sasa ni mume na mke.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz