Unaambiwa Aliyekutwa Katika Tairi la Ndege Uholanzi ni Mkenya - EDUSPORTSTZ

Latest

Unaambiwa Aliyekutwa Katika Tairi la Ndege Uholanzi ni MkenyaMaafisa wa polisi wa Uholanzi wamethibitisha kwamba mtu aliyekutwa katika tairi la ndege katika uwanja wa ndege wa Schipholni raia wa Kenya mwenye umri wa miaka 22.

Anapanga kuwasilisha ombi la kuchukua hifadhi nchini Uholanzi.

Mtu huyo alipatikana akiwa hai na kuwa na uwezo wa kuzungumza.Kwasasa anapokea matibabu katika hospitali moja.

Alikutwa katika tairi la ndege ya Cargolux baada ya ndege hiyo kusafiri kutoka Johhanesburg hadi nchini Uholanzi kupitia Nairobi Kenya.


Msemaji wa jeshi la polisi nchini Uholanzi aliambia BBC , inatarajiwa kwamba ataomba hifadhinchini Uholanzi , lakini kwasasa hali yake ya kiafya ndio muhimu.

Sio kawaida kwa stowaway katika safari za mwendo ,mrefu kukutwa wakiwa hai, kutokana na baridi kali na upungufu wa hewa ya oksijeni angani.

Maafisa wa polisi wa Uholanzi wanachunguza iwapo alijificha katika tairi hilo akiwa nchini Afrika kusini au Kenya.


Katika kipindi cha miaka mitano , watu saba waligunduliwa katika ndege hizo za Uholanzi na ni wawili pekee waliokutwa wakiwa hai.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz