Sallam SK Ajipa Ujiko TENA, Adai Ndio Aliyeunganisha Collabo ya Ali Kiba na Sarkodie - EDUSPORTSTZ

Latest

Sallam SK Ajipa Ujiko TENA, Adai Ndio Aliyeunganisha Collabo ya Ali Kiba na Sarkodie

 


Kwenye list ya nyimbo zinazo patikana kwenye Albamu ya The Only One King iliyotoka October 2021, utakutana na kolabo inayoitwa Happy ambayo Alikiba (35) amemshirikisha Rapa toka Ghana, Sarkodie (36)


Kwa mujibu wa Sallam Sk, Meneja wa Diamond kupitia kipindi cha The Joint,amedai ile kolabo ilitokea baada ya yeye kukutana na Sarkodie na wakawa wanapata Sigara mahali,ndipo Sarkodie Alipomwambia Sallam kuwa kuna msanii tokea Bongo anaitwa Alikiba ameMD ili wafanye kolabo, ndipo Sallam SK alimwambia ni kweli jamaa anafanya poa,Nenda kafanye jambo.


Kwenye hili pia Mwarabu kajipa Credits kuwa ameunganisha hii Kolabo na hakutaka malipo, Inafikirisha kuwa maneno ya Sallam Sk yawe makubwa zaidi kuliko Kazi za Alikiba, kweli sigara mbaya aisee na uzuri Madee kamchana Live kuwa ipo siku Mendez atakatwa makofi hadharani akiendelea na hizi sifa za kijinga, jamaa bado hajasahau alicho mfanyia Mombasa kumchomolea waya kwenye show ya Wizkid,leo hii anajifanya mwema na panga mfukoni.


Alikiba Kamleta Patoranking nchini, kabla ya Kuondoka tayari Pato kafanya kolabo na Nandy, Jux, G. Nako n.k, kesho Alikiba ajitambe eti yeye ndiye mfanikisha kolabo hizo? Kumleta mtu sehemu ni jambo lingine na kufanya kolabo na mtu ni jambo lingine pia,linategemea sana ushawishi wa anayetaka kufanya kolabo.

Hopetyga

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz