Radi Yaua Watu zaidi ya Watano.... - EDUSPORTSTZ

Latest

Radi Yaua Watu zaidi ya Watano....


Mtu mmoja anayefahamika Kwa jina la John Rajabu (60) Mkazi wa mtaa wa Bushabani kata ya Kibirizi Manispaa ya Kigoma ujiji Mkoani Kigoma amefariki baada ya kupigwa na Radi akiwa nyumbani kwake jana asubuhi.


Radi hiyo ambayo inasadikiwa kupenya katika ukuta na kumkuta akiwa ndani na kumchoma


Huko mkoani Mbeya watu wanne walifariki dunia papo hapo na mwingine kujeruhiwa baada ya kupigwa na radi katika Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.


Watu hao walipigwa na radi Jumapili Januari 9, 2022 wakichimba kaburi kwa ajili ya kumzika ndugu yao aliyefariki Januari 7.


Katika hali nyingine Mvua ya upepo iliyonyesha juzi katika Kata ya Ndolwa, Halmashauri ya Wilaya Handeni, mkoani Tanga imezua paa za vyumba vya madarasa manne na ofisi ya Shule ya Msingi Luye iliyopo Kata hiyo.


Akizungumza, Januari 21, 2022 Mkuu wa Wilaya ua Handeni, Siriel Mchembe amewahakikishia wazazi na wanafunzi ndani ya wiki mbili ukarabati utakuwa umekamilika.


Mchembe amesema vyumba vine vya madarasa pamoja na ofisi ya walimu vimeezuliwa na paa hivyo amewataka wananchi kushirikiana na Serikali kuhakikisha ukarabati unafanyika haraka.


“Timu ya mkurugenzi imeshapita na kufanya tathimini  ya vitu ambavyo vinahitajika,hivyo mkurugenzi amenihakikishia ndani ya siku 14 wanafunzi watarudi darasani na wengine wataendelea na masomo kwenye shule shikizi ya jirani,” amesema Mchembe.


Akielezea hali hiyo mwalimu mkuu wa shule ya msingi Luye, Hossein Mwesange amesema saa nane mchana ilitokea mvua kubwa iliyoambatana na upepo na kuezua madarasa hayo ila hakuna mwanafunzi wala mwalimu aliyeathirika


Amesema wanafunzi 300 watakosa masomo kwa zaidi ya wiki moja kutokana na madhara hayo, kwani hakuna madarasa ya ziada ambayo wataweza kusoma.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz