Kinachosabisha ndoa za “Babu na Mjukuu” - EDUSPORTSTZ

Latest

Kinachosabisha ndoa za “Babu na Mjukuu”

 


Katika maisha neno ‘ndoa’ linabaki na maana ileile ambayo ni kiunganishi kati ya watu wa wawili wanaounganishwa na msamiati wa ‘Mapenzi’ lakini kwa ubia wao huunganishwa kiimani, kimila na kiutamaduni wakiwekeana nadhiri ya kuwa pamoja katika shida na raha.


Hata hivyo wataalamu wa maisha na watu waliobobea zaidi katika masuala ya saikolojia wao huenda mbali zaidi na kusema kuna mengi zaidi katika tafsiri ya ndoa kuliko kuongelea mapenzi pekee.


Katika tafsiri hii mpya inayoongoza Maisha na ikaleta Ndoa za kustaajabisha ndio kumekuwa na matukio yanayobezwa au kukosolewa sana ya wanaume wazee kiumri, kuoa wake wa umri wa chini sana. Mathalani Mzee wa miaka 65 au zaidi anaoa mke wa miaka 25 nakuendelea au hata chini kidogo.


Wapo pia wanawake ambao ni watu wazima zaidi kuolewa na wanaume ambao ni vijana labda unaweza kuwaita wajukuu zao lakini wanaunganishwa na msamiati ‘Ndoa’

Ndani ya jamii zetu za kawaida ndoa hizi zinatokea mara nyingi tu na zinakuwa Gumzo hata kwa vyombo vya habari ambapo wataalamu wa masuala ya ustawi wa jamii wanasema Ndoa hizi zinzweza kuwa sababu ya uchumi, Umasikini, Tamaa, mikumbo na maumivu ya mapenzi ambayo mmoja anakua ameyapitia katika maisha yake.


Mzee Cal. Mika Metili (78) akiwa na mkewe mpya (27) amefunga ndoa hivi karibuni katika kanisa la KKKT usharika wa Ilboru, Januari 9, 2022. Wawili hao walianza mahusiano muda mrefu na hivi karibuni wamefanya utaratibu wa kurudi kundini na kubatiza mtoto wao wa miezi 7. Mke wa kwanza wa Col. Metili alifariki 2021 kwa tatizo la upumuaji.

Wapo watu marufu duniani waliooa wake wadogo sana kiumri, kwa uchache tu ni Nabii Ibrahim na mjakazi wa Misri, Raisi Trump, Mzee Mwinyi, Dkt Mengi na hivi majuzi na Mzee profesa Kapuya, kwa uchache.


Ingawa wapo watu maarufu pia ambao wameingia katika ndoa za aina hii, wapo wanajamii ambao wanapinga aina hizi za noda wakisema kuwa ni ndoa ambazo zinachangia kumaliza uhai wa mmoja ambae ni mzee zaidi haswa mzee huyu akiwa ni mwanaume.


Mara nyingi ndani ya ndoa hizi huwa hakuna kuendelea na uzazi haswa Mwanamke akiwa mtu mzima zaidi kwa sababu anakua ameshapita ule umri wa kupata mtoto.


Hata hivyo wataalamu wa malezi wanasema ndoa hizi zinakosa malezi mazuri kwa watoto kwa sababu ya utofauti wa fikra na uzoefu wa maisha kati ya wahusika.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz