AY Ajibu Tuhuma za Kumbania Collabo MB Dogo Kwa Juacali "Nisinge Jitoa Mimi Game ya Bongo Flava Ungekuwa Kama ya Malawi" - EDUSPORTSTZ

Latest

AY Ajibu Tuhuma za Kumbania Collabo MB Dogo Kwa Juacali "Nisinge Jitoa Mimi Game ya Bongo Flava Ungekuwa Kama ya Malawi"


Hi

Wiki hii ilianza kwa kasi baada ya majibizano makali kati ya Meneja wa Diamond Platnumz, Sallam Sk na Rapa Joh Makini kutokana na maneno ya Sallam Sk kwenye kipindi cha The Joint kuwa yeye ndiye aliyehusika kwenye kolabo ya A.K.A na Mwamba wa Kaskazini, kitu ambacho Joh Makini alikikataa na kusema Sallam ni moja ya watu waliokuwa wakipigana mchongo huo ukwame ila Mungu alipanga itokee.

Ishu hiyo pia ilimfanya Hit Maker wa Latifa, Mb Dogg kumtuhumu A.Y (MASTA) kama moja ya watu waliowahi kumbania kwenye game,2008 akimbania kufanikisha kolabo yake na msanii Jua Cal tokea +254 Kenya, Komenti ya Mb Dogg ikapostiwa Instagram kwenye ukurasa wa Fid Q, Na A.Y akatoa maoni na baadhi ya maneno akisema kama hasingejitoa kwaajili ya Game hii ya Bongo Flava basi kwasasa Muziki wa Bongo ungekuwa kama wa Malawi,huku akidai watu hawana shukrani.

Ikumbukwe A.Y ndiye msanii wa Kwanza tokea Tanzania kuanza kufanya Kolabo na wasanii wa nje(international Collaboration),akianza kufanya kazi na wasanii wa Kenya,kisha akaenda hadi Nigeria akifanya kolabo na wasanii kama J.Martin, P Square na mwanadada,marehemu Goldie Harvey. Hakuishia hapo tu, AY alifanya kolabo na wasanii tokea Jamaica,waishio Marekani kama Kingstone pamoja na Mis Trinity.

Hadi Kesho, A.Y atabaki kuwa Icon kwenye muziki wa Bongo Flava,muhasisi wa kolabo za nje Kijiti ambacho kimepokelewa vizuri na wasanii wengine kama Diamond,Alikiba, Harmonize,n.k Lakini pia aliwawezesha wasanii kibao tu wa Bongo kufanya kolabo na wasanii wa nje,akiwemo FA,Ommy Dimpoz,Diamond n.k

By Sajomedia
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz