Abiria aliyegoma kuvaa barakoa asababisha ndege kukatisha safari angani - EDUSPORTSTZ

Latest

Abiria aliyegoma kuvaa barakoa asababisha ndege kukatisha safari angani
Kampuni ya ndege ya Marekani -American Airlines iliyokuwa ikisafiri kutoka Miami kuelekea London Uingereza imelazimika kurudi ilikotoka kwasababu mmoja wa wasafiri wake alikataa kuvaa barakoa, imesema ndege hiyo.

American Airlines Flight to London Turns Back After Woman Refuses to Wear  Mask
Ndege ya American Airlines chapa AAL38 yenye wasafiri 129 ndani yake ilirejea Miami ambako ilikutana na polisi, ilisema.

Polisi walimsindikiza mwanamke mwenye miaka 40 na ushee kumuondoa ndani ya ndege hiyo, taarifa zinasema.

Mwanamke huyo amewekwa kwenye orodha ya watu wanaozuiwa kusafiri kwa ndege ya American Airlines, hadi uchunguzi wa kisa hicho utakapokamilika, imesema kampuni hiyo ya ndege.


 
Ndege hiyo ililazimika kukatiza safari yake na kurejea Miami Jumatano baada ya kusafiri kwa muda wa chini ya saa moja, kulingana na rekodi ya taarifa za safari ya kampuni hiyo.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz