Mkubwa Fella Adai Hakuna Msanii Anastahili Kulinganishwa na Diamond Platnumz Bongo - EDUSPORTSTZ

Latest

Mkubwa Fella Adai Hakuna Msanii Anastahili Kulinganishwa na Diamond Platnumz Bongo

 


Meneja wa Diamond Platnumz, Mkubwa Fella amesisitiza kwamba mwanamuziki anayewakilisha ndiye kigogo wa muziki nchini Tanzania.

Akiwa kwenye mahojiano ya hivi majuzi na Mbengo TV, Fella ambaye pia ni mwanasiasa alisema kwa sasa hakuna mwanamuziki anayestahiki kulinganishwa na Diamond Platnumz kote Bongo.

Meneja huyo aliwasihi Watanzania waache kujaribu kumshindanisha Diamond na wanamuziki wengine wa Bongo huku akisema kiwango chake ni cha kimataifa.

"Diamond ashindanishwe na mtu ambaye anaweza kustahiki kushindanishwa naye. Hapa Bongo jamani watu waache kwanza. Huko mwanzo tulikuwa tunatafuta numba, lakini sasa hivi ashakuwa mwakilishi wa taifa letu. Lazima tuwe wapana kidogo kuzungumzia hili. Tusiseme kwamba anaweza kashindanishwa na mtu fulani, hamna!" Fella alisema.

Fella alidai hata mmiliki wa lebo ya Konde Music Worldwide, Harmonize hajatosha mboga kuwekwa katika nafasi moja na bosi wake wa zamani.

"Watu wakimshindanisha Harmonize na Naseeb wanafeli. Harmonize ametengenezwa na Naseeb. Harmonize ana nafasi yake na Diamond ana nafasi yake zaidi. Diamond kwa Harmonize anasimama kama baba. Ukimfananisha mtu na babake ni uongo" Alisema Fella.


HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIALDOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

Fella hata hivyo alimkubali Harmonize kama msanii mkubwa ambaye anafanya vizuri katika nafasi yake

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz