Maskini Wakazi..Akatishwa Tamaa na Muziki wa Hip Hop Tanzania "Tumepoteza Mvuto Kibiashara" - EDUSPORTSTZ

Latest

Maskini Wakazi..Akatishwa Tamaa na Muziki wa Hip Hop Tanzania "Tumepoteza Mvuto Kibiashara"


Rapa Wakazi amefunguka kuhusu hali ya muziki wa Hip Hop kwa sasa hapa nchini, amesema wasanii wa Hip Hop Tanzania wamepoteza mvuto wa Kibiashara hivyo ni ngumu kwa wawekezaji kuwadhamini. Wakazi amefunguka hayo wakati akijibu tweet ya mdau mmoja ambaye alitoa pendekezo kwamba, anatamani kufanyika kwa onesho moja kubwa la Hip Hop mwezi huu. 


Aidha @wakazi ambaye amekuwa akipaza sauti na kutoa mitazamo yake kwenye mambo mbali mbali, aliongeza kwamba hata kampuni moja ya bia ambayo imekuwa ikiupa nguvu muziki wa Hip Hop, mwaka huu wamehamia kwa Ma-DJ na sio wasanii wa Hip Hop kutokana na kukosa weledi na uwezo wa Kibiashara nyuma ya wasanii wa Singeli na Bongo fleva.





Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz