Juma Lokole "Umbea Una Mwisho Tumeamua Kujiongeza" - EDUSPORTSTZ

Latest

Juma Lokole "Umbea Una Mwisho Tumeamua Kujiongeza"


Jopo zima la watangazaji wanaounda kipindi cha ICU, (Jopo la Wambea) ambao ni Juma Lokole, Kwisa na Maimartha, Desemba 9, 2021 wameweka wazi kuwa mambo ya kufukunyua vitu vya watu vina mwisho hivyo kwa sasa wameamua kujiongeza baada ya kupata dili la ubalozi wa ufugaji kuku na kilimo.

Dili hilo nono la kufungia mwaka, wambea hao wamelipata kutoka kwa Mr Kuku, mwenye mradi huo mkubwa uliopo Kibada, Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Juma Lokole amesema kuwa, mambo ya umbea yana mwisho hivyo wameona wajiingize kwenye mambo ya maendeleo yanayoweza kuwapa faida kubwa huko mbeleni.

"Mwezangu umbea nao una mwisho wake kwa kweli sasa tumeamua kuwekeza mashambani na kwenye ufugaji wa kuku ambao kazi yetu ni kula faida tu," alisema Juma Lokole.


Habari @imeldamtema
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz