Hakuna Ubishi..Konde sasa ni Mkubwa kwa Jina, Kimwili na Kisanii. Yes! Ametafuna Mfupa Uliowashinda Wengi - EDUSPORTSTZ

Latest

Hakuna Ubishi..Konde sasa ni Mkubwa kwa Jina, Kimwili na Kisanii. Yes! Ametafuna Mfupa Uliowashinda Wengi


Ukimtazama wa kwenye BSS, akitolewa nishai na kina Master Jay pamoja na Salama. Ilikuwa vigumu kuamini kuwa siku za usoni atakuwa msanii namba moja wa WCB.

Miaka kadhaa mbele akawa katikati ya Mondi ya Kiba kisanii. Mkubwa mbele ya wakubwa. Mwanzo ni kama aliiga mitambao ya Mondi na njia zake. Ghafla kikaibuka kiumbe kingine cha tofauti kabisa.

Huu ni ubishi wenye matokeo chanya. Konde sasa ni mkubwa kwa jina, kimwili na kisanii. Yes! Ametafuna mfupa uliowashinda wengi. Dunia hii kujitoa mikononi msanii ‘fotefiti’ kama Mondi na kusonga siyo jambo dogo.

Katikati ya magwiji wa hizi mishe Fella, Tale na Sallam SK. Mmakonde kasimama na michongo inaendelea kupita kwenye njia zake kama kawa. Yupo nao katika mstari mmoja. Ogopa sana. Heshimu.

Konde yuko vizuri sana kuandika, kuimba na jukwaani. Sifa hizi wasanii wengi tena wakubwa lakini hawana uwezo huo kwa sasa. Ukitaka kuamini Konde Boy ni noma ulizia Rich Mavoko na Aslay walipo.

Hata shoo alizopiga kwa muda mfupi. Utaamini kuwa anawazidi kaka na wadogo zake wengi wa sasa. Na Ijumaa hii yupo Viwanja vya Posta pale Kijitonyama kwenye Freshers Bash.

Mwamba ni mtawala kwa sasa…

Na @dklevy_






Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz