Unaambiwa...Jack Patrick Kuzima Mastaa wa Kike Bongo, Huyu Ndo Original Bosslady - EDUSPORTSTZ

Latest

Unaambiwa...Jack Patrick Kuzima Mastaa wa Kike Bongo, Huyu Ndo Original Bosslady
ALIYEKUWA video vixen (muuza nyago) maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick almaarufu Jack Patrick ametoka jela baada ya kukaa miaka nane gerezani nchini China na sasa anakwenda kuzima kabisa mbwembwe za mastaa wote wa kike Bongo.


Jack Patrick ambaye alinogesha vilivyo video za wasanii wa Bongo Fleva kama She Got A Gwan ya marehemu Ngwea na Nataka Kulewa ya Diamond Platnumz alikamatwa Desemba 19, 2013.


Jack alikutwa na dawa za kulevya aina ya Heroin zenye uzito wa kilo 1.1 katika Uwanja wa Ndege wa Macau akitokea jijini Bangkok nchini Thailand kuelekea Guangzhou; Mji Mkuu wa Jimbo la Guangdong Kusini mwa China.


Kabla ya kukamatwa na kufungwa, Jack ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa msanii Juma Jux kabla ya kuolewa na tajiri, ndiye aliyekuwa staa orijino, tofauti na hawa wa sasa ambao wengi wanafeki maisha.


Miaka kumi iliyopita, Jack ndiye aliyeanzisha jina la boss lady kabla ya ma-boss lady wote unaowajua kutokana na aina ya maisha ya kifahari aliyokuwa akiishi kuanzia mavazi ya thamani, mikufu, nyumba na magari ya kifahari; ndiye staa wa kike wa kwanza Bongo kumiliki gari la bei mbaya aina ya Mercedes Benz.


Unaambiwa huyu, Jack ndiye queen wa ma-queen aliyekuwa mrembo wa mfano kwa warembo kibao Bongo wakiwemo akina Hamisa Mobeto.


Sasa amerejea umri ukiwa umesonga, lakini bado anawaka na wale wanaotisha kwa kula bata kama Irene Uwoya, wanaambiwa wakae kwa kutulia.

Habari za ndani zinasema bado utajiri wake anao kwani haukusambaratika yakiwemo magari na mjengo wa kifahari jijini Dar.


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz