Kimesanuka..Kumbe JPM Ndio Alisaidia Harmonize Kuachiwa Awe Huru na Lebo ya WCB Baada ya Kumzungusha Muda Mrefu - EDUSPORTSTZ

Latest

Kimesanuka..Kumbe JPM Ndio Alisaidia Harmonize Kuachiwa Awe Huru na Lebo ya WCB Baada ya Kumzungusha Muda MrefuSakata la mwanamuziki @harmonize_tz na @diamondplatnumz linaendelea kuchukua sura mpya , kila baada ya Uchambuzi wa kile ambacho amekizungumza mapema leo hii uwanja wa ndege baada ya kurejea kutoka nchini marekani

Katika maelezo mengi aliyofunguka msanii Harmonize kuhusu ugomvi wake na msanii mwenzake diamond platnumz, amemtaja aliyekua raisi wa awamu ya 5 wa Tanzana hayati John Magufuli kama mtu aliyemsadia kupata mkataba wake wa kujitoa katika record label ya WCB Wasafi

Harmonize amemuelezea hayati Magufuli kama kiongozi wa ngazi ya juu ambae aliamua kumsaidia baada ya kumueleza matatizo yake na msanii mwenzake, ambapo alipiga simu uwanja wa ndege kuzuia safari ya diamond platnumz kuelekea marekani mpaka pale atakapo kamilisha kumpatia mkataba wa kujitoa WCB ambao ulikua tayari ila alikua akicheleweshwa kuupata


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz