Harmonize "Natumaini Urafiki Wangu na Kajala Masanja Utarejea" - EDUSPORTSTZ

Latest

Harmonize "Natumaini Urafiki Wangu na Kajala Masanja Utarejea"

 


Hivi majuzi mwanamuziki Rajab Abdul Kahali almaarufu kama Harmonize alizindua albamu yake ya pili 'High School'.

Staa huyo wa Bongo alitumia ukurasa wake wa Instagram kufafanulia mashabiki wake maana ya nyimbo ishirini zilizo kwenye albamu yake mpya.

Harmonize alisema wimbo nambari saba katika albamu yake mpya 'Mtaje' ambao aliandikia aliyekuwa mpenzi wake Kajala Masanja ndio ulikuwa wa kihisia zaidi.

Alimtambua mchumba huyo wake wa hivi karibuni kama mtu aliyemuonyesha mapenzi zaidi na kumuelewa vizuri huku akimuomba msamaha kwa mabaya aliyomfanyia.

"Samahani kama nitaumiza yeyote. Kajala alinijua zaidi. Alikuwa anajua mimi ni mtu wa aina gani na napenda nini kwa wakati gani. Naamini alikuwa ananifahamu vizuri. Niamini, sitaki kuenda zaidi kueleza ilivyokuwa lakini nataka kuchukua fursa hii kama mwanaume kumuomba msamaha. Nahisi kilichofanyika ni mimi nilisababisha.Sipendezwi na kilichotokea kama mwanaume. Mimi ni mwanaume, lawama zote zije kwangu" Alisema Harmonize.


Konde Boy alisema hakuwahi kuwa na chuki yoyote kwa binti ya Kajala, Paula huku akidai alimpenda kama mtoto wake tu.

Alisema anajuta yote ambayo yalitokea kati yake na Kajala kuhusiana na bintiye huku akimsifia kama mama bora.

"Haijalishi nini, sikufaa kureacti vile. Nahisi vibaya sana. Naona niliingiza mtu kwenye matatizo, mambo ya kupelekana kwa polisi. Nimefanya aonekane sio mama bora. Ninachoamini na najua, Kajala alikuwa anajaribu sana kwa binti yake. Alijaribu sana kumfanya bintiye bora. Naamini yeye ni mzuri" Harmonize alisema.

Alisema anaamini kuwa kufikia sasa mama ya mpenzi wa Rayvanny tayari ameuguza maumivu na anaamini kwamba atasamehewa.

"Tulikuwa na hadithi nzuri ya mapenzi pamoja. Tulipendana sana na kila mtu anajua. Huwezi sema hatukupendana. Akiniambia kitu nilikuwa nafanya. Alinibadilisha. Alifanya mengi sana" Alisema.

Konde Boy alimtakia Kajala mafanikio mazuri maishani huku akisema anatumai siku moja urafiki wao utarejea.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz