Unaambiwa Viatu vya Michael Jordan Vyapigwa Mnada, Vyauzwa Kwa Shilingi Billion 3 - EDUSPORTSTZ

Latest

Unaambiwa Viatu vya Michael Jordan Vyapigwa Mnada, Vyauzwa Kwa Shilingi Billion 3




Viatu vya aliyekuwa mchezaji nyota wa timu ya kikapu nchini Marekani Michael Jordan vimeuzwa kwa bei ya $1.47m (£1.1m) sawa na Tsh bil 3,227,000,000 iliovunja rekodi katika mnada.



Jordan alitumia viatu hivyo aina ya Nike Air Ships vyenye rangi nyekundu na nyeupe wakati wa msimu wake wa kwanza akiichezea timu ya Chicago Bulls.

Huo ndio mwaka yeye na Nike walianza ushirikiano wao kuunda nguo zenye nembo yake na viatu. Bei hiyo ndio ya juu zaidi kwa viatu vya michezo.

Jordan anaaminika na wengi kuwa mchezaji bora zaidi katika historia ya mchezo wa vikapu.Jordan ambaye kipindi kirefu aliichezea timu ya Chicago Bulls alikuwa nyota na kuweza kuinua kiwango cha mchezo huo kote duniani.

Jordan ambaye alistaafu mwaka 2003 alikuwa mchezaji wa kwanza bilionea katika historia ya NBA .





Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz