Unaambiwa Mimba ya Malkia Karen Bado Utata Mtupu - EDUSPORTSTZ

Latest

Unaambiwa Mimba ya Malkia Karen Bado Utata Mtupu


Siyo stori kwamba, mrembo kunako Bongo Fleva, Malkia Karen ni mjamzito wa miezi mingi akikaribia kabisa kujifungua baada ya wadukuzi kumnyemelea na kumrekodi video akifanya mazoezi kama ilivyo kwa wajawazito ambapo hushauriwa na madaktari kufanya mazoezi.

Lakini swali kubwa linalozua utata ni juu ya ni nani hasa ni mmiliki wa mimba hiyo ya Karen?

Mastaa wawili wa Bongo Fleva wanatajwatajwa sana; si wengine bali ni Diamond Platnumz na Rayvanny.

Kwa nini wawili hao? Kwa sababu kuna mawasiliano ya karibu kati yao na mwanadada huyo ambaye kimsingi yupo kwenye levo za akina Paula Kajala na Sonia, lakini hazungumzwi sana, labda kama watu wanamhofia baba yake, Gardner G Habash.

Hata hivyo, ili kutengua kitendawili hicho ni vyema kusubiri Karen ajifungue kila kitu kitajulikana.

Lakini habari za ndanindani sana, wahusika siyo Diamond wala Rayvanny!
Cc; @sifaelpaul
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz