Shilole Acharuka "Shishi ni Brand Kubwa Internationally Siwezi Jibishana na Mtu Mitandaoni, Event ya Kiba ilihitaji Watu Wakubwa" - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Shilole Acharuka "Shishi ni Brand Kubwa Internationally Siwezi Jibishana na Mtu Mitandaoni, Event ya Kiba ilihitaji Watu Wakubwa"
Msanii wa muziki wa Bongo Flava na mmiliki wa mgahawa wa Shishi Food, @officialshilole amedai hawezi jibizana na mtu mitandaoni kiholela holela tu maana yeye ni brand kubwa sasa hivi.

Hii imekuja baada ya kile kilichotokea kwenye Listening Party ya Albamu ya Alikiba ya ONLY ONE KING October 6 mwaka huu,kuonekana Shilole akipewa Shavu kubwa zaidi kwenye event hiyo kuliko Esha Buheti ambaye amekuwa akimpush Alikiba kwa muda mrefu.

Wawili hawa wote ni wafanya biashara ya chakula, hivyo Inasemeka hicho pia kimechagiza zaidi tofauti baina yao hadi kufikia hatua ya Esha kujitoa kuwa kama shabiki kwa Alikiba.

Hasa kwenye camera za Refresh ya Wasafi Tv, Shishi amedai hawezi bishana na Esha, kwanza hajui kama hilo jambo lina ukweli ndani yake, na kama ni hivyo lazima Esha ajue Event ya Alikiba ilihitaji watu wakubwa,na Alikiba akafanya hivyo kumualika yeye kama msanii mkubwa na kama dada yake ,na pia Brand ya Shishi sio ya kujibizana hovyo na watu mitandaoni. Kingine Kawazidi followers wote wawili,hivyo Shishi ni Brand kubwa internationally
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz