Rihanna Atubu Kwa Flaviana Matata, Aamua Kumfollow Instagram - EDUSPORTSTZ

Latest

Rihanna Atubu Kwa Flaviana Matata, Aamua Kumfollow Instagram


Mwanamitindo wa Kimataifa kutokea Tanzania anayefanya shughuli zake New York nchini Marekani, anagonga vichwa vya habari mara baada ya Mwimbaji maarufu duniani, Rihanna kum-follow kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Mwaka 2013 Flaviana alitajwa na Jarida la Forbes Africa kuwa ni miongoni mwa Wanamitindo wanaolipwa fedha nyingi zaidi, huku mwaka 2017 akitajwa na Okay.com kuwa miongoni mwa wanawake 100 bora Afrika.

Rihanna toka Marekani ana followers zaidi ya milioni 109, huku Flaviana akiwa nao milioni 1.7 kwenye mtandao huo ulioanzishwa Oktoba 2010 na sasa unamilikiwa na kampuni ya Facebook.

Katika kazi yake ya mitindo Flaviana amefanikiwa kusafiri katika nchi mbalimbali na kukutana na mastaa wakubwa kama Jay Z na mkewe, Beyonce.

Hadi sasa Flaviana amefanikiwa kutunukiwa tuzo kama Arise Fashion Magazine Awards (2011), Nigeria Next Super Model Awards (2012), Africa Diaspora Awards (2012), Swahili Fashion Week Awards (2012), Malkia wa Nguvu Awards (206) na Global Woman Gala (2018).

Mrembo huyo ambaye mwaka 2007 alishinda taji la Miss Universe Tanzania, kupitia taasisi yake ya Flaviana Matata Foundation (FMF) amekuwa akitoa misaada ya vifaa na ada hasa kwa wanafunzi wa kike nchini Tanzania.

Flaviana Matata Foundation ilizinduliwa Juni 2011 ikiwa na lengo la kuanzisha mfuko wa kusaidia elimu ya watoto waishio katika mazingira magumu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

Kwa Habari Zaidi, Usiache Kutembelea na Ku-Subscribe Youtube Channel Yetu Ya πŸ‘‰ #UswazTv

Follow Now πŸ‘‰ @UswazTv.




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz