elru87tYGBGEm Rais Joe Biden akutana na Papa Francis Muungwana - EDUSPORTSTZ

Latest

Rais Joe Biden akutana na Papa Francis Muungwana

 




Rais Joe Biden wa Marekani amekutana na kiongozi wa kanisa Katoli Papa Francis na kujadiliana mabadiliko ya tabianchi na janga la COVID-19, na kuzungumza na Emmanuel Macron kuhusu namna ya kuimarisha upya mahusiano yao.
Rais Joe Biden wa Marekani amekutana na kiongozi wa kanisa Katoliki duniani, Papa Francis huko Vatican City na kuzungumza naye changamoto za kiulimwengu kuanzia janga la COVID-19 hadi mabadiliko ya tabianchi na umasikini.

Kabla hajaondoka Vatican, ikulu ya Marekani ya White House ilisema Biden alimshukuru Papa Francis kwa namna anavyopigania mapambano dhidi ya umasikini duniani na wale wanaouteseka kwa njaa, mizozo na mauaji.

Hii ni mara ya kwanza kwa rais Biden kukutana na kufanya mazungumzo na Papa Francis, tangu alipochaguliwa kuwa rais mapema mwaka jana.

Biden, ambaye ni kiongozi wa pili wa imani ya Kikatoliki katika historia ya Marekani baada ya John F. Kennedy, ni muumini safi ambaye hakosi kuhudhuria ibada za kila Jumapili.

Kiongozi huyo amekuwa akizungumzia namna imani yake ilivyomsaidia na kumpa ujasiri katika majanga mbalimba kama ya kifo cha mkewe wa kwanza na bintiye katika ajali ya gari na baadae kijana wake Beau, aliyefariki kutokana na maradhi ya saratani.

Lakini licha ya Papa Francis na Biden kukubaliana katika masuala fulani, bado wakuu hao wamejikuta wakitifautiana katika mambo kadhaa kama ya utoaji wa mimba. Biden anaunga mkono haki ya utoaji mimba, lakini Papa Francis anapingana nayo kwa kuwa anasema utoaji mimba ni uuaji.

Rais Joe Biden na rais Emmanuel Macron walipokutana pembezoni mwa mkutano wa G20mjini Rome kujadiliana kuhusu kurejesha mahusiano baina yao.

Ijumaa jioni, Biden alikutana na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwenye mkutano wa mataifa yaliyoendeleana yanayoinukia kiuchumi ya G20 mjini Rome na kusema Marekani haina mshirika wa muda mrefu na mwaminifu zaidi ya Ufaransa. Biden yuko Rome kuhudhuria mkutano huo wa kilele wa G20 na baadaye kwenye Glasgow, Scotland kuhudhuria mkutano wa kilele wa mabadiliko ya hali ya hewa, COP26.

Kwenye mkutano na Macron, Biden alisema hakuna mahali ambapo Marekani haitashirikiana na Ufaransa, wakati mataifa hayo yakiangazia namna ya kujadiliana kuvurugika kwa mahusiano baina yao, baada ya Australia kuvunja mkataba na Ufaransa wa kununua nyambizi, na badala yake kuingia mkataba mpya na Marekani na Uingereza.

Biden alimwambia Macron kwamba anahisi mkataba huo ulifikiwa kihuni na hakukua na uaminifu.

Macron alisema washirika hao wawili wataendeleza ushirikiano thabiti ili kuzuia hali ya kutoelewana kutokea tena. "Kitu ha msingi kwa sasa ni kile ambacho tutakifanya pamoja katika wiki, miezi na miaka ijayo" alisema Macron.

Biden anatarajiwa pia kukutana na mwenyeji wa mkutano huo wa kilele wa G20, rais wa Italia Sergio Matarella na waziri mkuu Mario Draghi.





Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz