Kiukweli soko la wasanii kwa Bongo bado halijawa kubwa kivile ukilinganisha na kile wanachofanya. Chukulia mfano Rapa kama @younglunya kwa muda ambao amekaa kwenye game kibongo bongo alafu muwazie angekuwa mambele angekuwa na mkwanja au mafanikio kiasi gani.
Wakati wanajaribu kupigania living standard zao kuna watu huko ndichi wanajiita mapromota wanatumia majina ya wasanii kupiga pesa. Hasa Young Lunya limemfika kooni na kutaka kudeal na Promota ambaye huko Songea amekaa mkao wa kutafuna pesa za mashabiki hii leo October 1 wakijua Young Lunya ni moja ya watumbizaji kati ya wasanii wanne waliotajwa. Lunya ameandika👇
“WATU WA SONGEA OGOPENI MATAPELI SIPO KWENYE HII SHOW ❌❌❌❌❌
MAPROMOTA MUWE NA HESHIMA NA KAZI ZA WATU, TUNAPITIA VITU VINGI SANA KWENYE KUTENGENEZA KAZI ZETU, HII SIO MARA YA KWANZA NAONA VITU KAMA HIVI, TUNASHINDWANA BEI THEN UNAENDA KUPROMOTE NITAKUWEPO SIO SAWA KABISA, NA HAWA WATAKUWA MFANO KWA WENGINE WATAKAOFANYA HIVI TENA. SANAA NI KAZI PIA KUWENI NA HESHIMA NA KAZI ZA WATU... @petitman_wakuache MALIZANA NAO HAWA TAFADHALI”
Meneja wa msanii huyo @petitman_wakuache amethibitisha kudeal na huyo mtu huku mtangazaji mkubwa Bongo ,@lilommy akikazia hatua za kisheria zichukuliwe.
“Inaonekana una demand Songea, fanyeni kuandaa show yenu ya kweli kweli mchele unawasubiri, halafu isiishie kuposti tu izo posters, jamaa hao washulikiwe vitu viende kisheria, kutumia jina na picha bila ridhaa na kudanganya watu, faini nzito iingie.”- Lil Ommy
Post a Comment