Nandy ni Diamond wa Kike..Hakubali Kushindwa Kuwafuata Mashabiki zake nje ya Nchi - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Nandy ni Diamond wa Kike..Hakubali Kushindwa Kuwafuata Mashabiki zake nje ya Nchi
SEXY lady kunako Bongo Fleva, Nandy The African Princess ameamua kuwafuata mashabiki wake huko nje ya nchi baada ya kuanika ratiba ya shoo zake katika kuufunga mwaka 2021.

Nandy anasema kuwa, anatarajia kufanya shoo zaidi ya 15 ndani ya nje ya nchi kabla ya mwaka kupinduka.

Anasema kuwa, shoo zake za kimataifa atazifanyia Nairobi nchini Kenya, Lagos nchini Nigeria, Dubai na Afrika Kusini.

Hatua hiyo ya Nandy inakuja baada ya hivi karibuni kutangaza ziara yake ya kimuziki nchini Marekani kuanzia Machi hadi Aprili 2022 baada ya kuihairisha kwa mwaka mmoja.

Utakumbuka mapema mwaka jana, Nandy alitangaza ziara yake iliyoipa jina la Nandy USA Tour 2020 ambayo ingeanza Mei 22 hadi Juni 20, 2020, lakini akalazimika kuifutilia mbali kufuatia mlipuko wa janga la UVIKO-19.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz