Mzimu wa Biashara za Wasanii Kufa Kifo Cha Mende Kipi Kimewapata? Mofaya, Chibu Perfume, Chibu Karanga na Fyne By Falsafa - EDUSPORTSTZ

Latest

Mzimu wa Biashara za Wasanii Kufa Kifo Cha Mende Kipi Kimewapata? Mofaya, Chibu Perfume, Chibu Karanga na Fyne By Falsafa


DELLABOSS.
Hii ni perfume ya @hajismanara , aliizindua kwa mbwembwe zote wakati akiwa msemaji wa @simbasctanzania Mastar kibao walihudhuria uzinduzi huo, Lakini hivi sasa hizo perfume kimya hata mwaka hazikumaliza.

MOFAYA.
Hiki ni kinywaji cha Alikiba, hii ni kama sijui kufata mkumbo maana tangu aizindue sikuwahi kukutana nayo kokote.(sijui ndio kusema hapendi show off)

CHIBU PERFUME.
Hii ni perfume ya Diamond. Hii nayo sioni chochote kikiendelea. Ila walio wahi kuitumia wanasema ni ya kawaida sana na bei ni kubwa mno(bei haiendani na bidhaa ni kama alikuwa anauzia jina)

CHIBU KARANGA.
Hizi pia alizindua Diamond lakini hivi sasa hazisikiki kabisa.

FYNEBYFALSAFA
Hii ni perfume ya Hamisi Mwijuma (mwana F.A), hii nayo sijui inaendeleaje. Siku hizi sioni hata matangazo yake, nahisi hazipo mjini.

Mnaweza kuongezea biashara zingine za hawa ndugu zetu zilizokufa kifo cha mende.

Je, huwa wanakwama wapi labda? Mbona Jux na Bdozen Biashara zao za nguo hazifi gafla kama hizi za wenzetu.

Tangaza Biashara yako Hapa, Piga Simu 0714604974

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz