Mauaji ya Agnes Wanjiru: familia ya Kenya wakasirishwa na Jeshi la Uingereza 'kuficha' ukweli - EDUSPORTSTZ

Latest

Mauaji ya Agnes Wanjiru: familia ya Kenya wakasirishwa na Jeshi la Uingereza 'kuficha' ukweli





Familia ya mwanamke mmoja wa Kenya anayedaiwa kuuawa na mwanajeshi wa Uingereza mwaka 2012, imeelezea BBC hasira zao na kukata tamaa kwao kwamba mpaka sasa hakuna hata mtu mmoja aliyepatikana na hatia ya mauaji hayo.

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imesema Uingereza inashirikiana na Kenya kuhusu kifo cha Agnes Wanjiru kufuatia tuhuma zilizotolewa na gazeti la Sunday Times kwamba kuna ukweli unafichwa.

Mwili wa Agness ulipatikana kwenye shimo la choo kwenye hoteli moja karibu miezi mitatu baada ya kufurahia pamoja akiwa na wanajeshi.

Kwa upande wake Balozi wa Uingereza nchini Kenya Bi. Jane Marriott ameandika kwenye kurasa ya twitter kwa kueleza masikitiko yake kwa familia ya Agnes na kuhakikishia Wakenya kuwa Uingereza itashirikiana na Kenya katika uchunguzi na kusaidia kukabiliana na tatizo hilo ipasavyo.

Binti huyo aliyekuwa na umri wa miaka 21, aliacha mtoto wa kike wa miezi mitano, ambaye kwa sasa analelewa na dada yake Rose Wanyua katika mji wa Nanyuki, kilometa 200km Kaskazini mwa mji mkuu, Nairobi.

Bi. Wanyua kwa uchungu huku akilia, alieleza jinsi taarifa ya gazeti la Sunday Times ilivyoibuka upya kumbukumbu za machungu.

Yeye na mumewe John Muchiri walisema kwamba familia hiyo imekata tamaa ya kupata haki kuhusu kifo cha Wanjiru, ambaye walikuwa wakimuita Ciru.

Kwa miaka 9 baada ya kifo cha mpendwa wao, familia ya Agnes Wanjiru – inasubiri kupata haki bila mafanikio.

 




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz