Machinga Barabarani Mwisho Leo, RC Makalla Atoa Tamko - EDUSPORTSTZ

Latest

Machinga Barabarani Mwisho Leo, RC Makalla Atoa Tamko




MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla amewataka Wafanyabiashara Wanaofanya biashara maeneo yaliyokatazwa hususani Kariakoo kufika Soko la Machinga Complex kwa ajili ya kupatiwa nafasi Kutokana na Soko hilo kusaliwa na nafasi 2,400 za Wafanyabiashara.

 

RC Makalla amesema hayo alipotembelea Soko hilo na kueleza kuwa mpaka Sasa Zaidi ya Wafanyabiashara 2,200 wamepatiwa maeneo ya kufanyia biashara na wanafurahia biashara zinakwenda vizuri sokoni apo.

 

Aidha, RC Makalla amesema Serikali imedhamiria kutatua changamoto zote za kibiashara kwenye maeneo walipopelekwa Wafanyabiashara ikiwa ni pamoja na kuelekeza LATRA kufikisha huduma ya Usafiri wa Daladala kwenye maeneo hayo ikiwemo Soko la Machinga ili kuchochea Biashara.

 

Hata hivyo RC Makalla amesema ifikapo siku ya kesho ndio mwisho wa watu kufanya biashara kwenye maeneo yaliyokatazwa Kutokana na muda wa siku 12 alizoongeza kufikia kikomo.

 

Pamoja na hayo RC Makalla amesema zoezi la kuwapanga vizuri Machinga kwa Mkoa huo linakwenda vizuri na kwa utulivu wa Hali ya juu Kutokana na elimu iliyotolewa na Serikali na Viongozi wa Machinga.

 




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz