Jumba la Kifahari la Kylie Jenner Balaa Tupu - EDUSPORTSTZ

Latest

Jumba la Kifahari la Kylie Jenner Balaa Tupu

Tazama picha za ndani za jumba la kifahari analomiliki Kylie Jenner (24) ambalo alilinunua kwa dola za Kimarekani $36.5 million ambazo ni zaidi ya bilioni 84 za Kitanzania.
 

Jumba hilo lipo Beverly Hills na lina vyumba 7 vya kulala, mabafu 14, apartments mbili za wageni, na vyumba vingine maalum kwa wageni wenye hadhi zao, jumba hilo lina swimming pool, uwanja wa michezo, gym, jiko la mpishi maalum(professional chef), nyumba ya mlinzi na mazagazaga mengine mengi ya kisasa.


Kylie ni staa wa vipindi vya TV ambaye pia amegeukia biashara ya vipodozi ambayo imempa mafanikio makubwa baada ya kuamua kuitumia vizuri mitandao ya kijamii kutangaza biashara zake.
 

Mrembo huyo anayetarajia kupata mtoto wa pili, Mwanzo kabisa alikuwa akitupia mapichapicha ya ajabu tu ili kupata kiki lakini baadaye akajiongeza kuitumia mitandao ya kijamii kikazi. Instagram pekee kwasasa followers zaidi ya milioni 278.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz