Huwezi Amini Hakuna Watu Wanaojikuta Wametoboa Maisha Hapa Mjini Kama Hawa Hapa - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Huwezi Amini Hakuna Watu Wanaojikuta Wametoboa Maisha Hapa Mjini Kama Hawa Hapa
-Wanaojua kuzungumza Kiingereza hata kama wanazungumza Kiingereza "broken". Wote ni mashahidi, hawa Siku zote hujihisi wao ni bora na maisha wameyapatia.

- Wanaomiliki matoleo mbalimbali ya simu za iPhone. Siongezi neno kuhusu kundi hili.

- Waliochukua mkondo wa masomo ya sayansi walipokuwa sekondari na baadaye wakaenda vyuo vikuu kusomea kozi mbalimbali za uhandisi. Hawa hata ukiwakuta mtaani bila ajira, wanajihisi tayari wameyapatia maisha.

- Wahitimu vijana wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Siongezi neno kuhusu kundi hili.

- Vijana wa Kitanzania ambao kwa wakati fulani waliwahi kuishi Marekani au Uingereza harafu kwa sasa wamerudi Bongo kupambana na msoto wa maisha.

- Wanaomiliki gari jamii ya Vitz, IST na Altezza. Jeuri na mikwara yao barabarani inatupa picha halisi.

- Wanajeshi vijana miezi yao kwanza kwenye ajira Jeshini harafu uwakute Uraiani wamevaa zile sare zao zenye mabaka mabaka.

Ongezea wengine unaowajua.

Karibuni.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz