Zari Hassan Ahusishwa na Utapeli Mwenyewe Ajitokeza na Kutoa Onyo Kali - EDUSPORTSTZ

Latest

Zari Hassan Ahusishwa na Utapeli Mwenyewe Ajitokeza na Kutoa Onyo Kali


Mfanyabiashara zarithebosslady amejitokeza kutoa tahadhari kwa wafuasi wake baada ya watu kuibuka na kutapeli watu kupitia jina lake na sura yake

Akizungumza kupitia video aliyoi-post Instagram Zari amesema kuwa kumekuwa kuna kundi la watu wanatapeliwa kupitia jina lake.

Watu hao wamekuwa wakiambiwa kuwa Zaria anafanya mafunzo ya biashara za sarafu mtandaoni Forex na wengine hutumia jina lake kuomba msaada kupitia taasisi yenye jina lake kwaajili ya kusaidia watu

"Nahitaji mfahamu sifanyi biashara, sifanyi Forex, sijaomba pesa kuwezesha taasisi yangu ya Zari Foundation"

"Sipeleki watu nje ya nchi kuwatafutia kazi. Watu wengi wamekuwa wakitapeliwa na lawama zinarudi kwangu kwasababu matapeli wamekuwa wakitumia sura yangu"

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz