Vanessa Mdee Apewa Onyo Kali na Mpenzi wa Zamani wa Rotimi - EDUSPORTSTZ

Latest

Vanessa Mdee Apewa Onyo Kali na Mpenzi wa Zamani wa Rotimi



Vanessa Mdee anaonywa na X wa Rotimi. Baada ya kutoa tangazo la ujauzito wake mapema wiki hii, Msanii mashuhuri kutoka Bongo Vanessa Mdee ameonywa kuwa asijipige kifua sana kuhusu mpenzi wake mwigizaji Olurotimi Akinosho almaarufu kama Rotimi.

Mtangazaji Kim Oprah kutoka Nigeria ambaye kwa wakati mmoja alichumbiana na Rotimi amemshauri Mdee asiwe starehe sana naye kwani hana uhakika kuwa atasalia kuwa malkia wake milele.

Kupitia ukurasa wake wa TikTok, Oprah amemweleza Mdee kuwa hata yeye kwa wakati mmoja alikuwa amekalia nafasi ambayo kwa sasa ameichukua na licha ya kuhakikishiwa kuwa yeye ni kila kitu kwake uhusiano wao haukudumu.

Oprah alitengeneza video ambayo ilionyesha picha mbili tofauti, moja ikionyesha Mdee akiwa pamoja na Rotimi huku nyingine akimuonyesha yeye akiwa pamoja na mwigizaji wakati walikuwa wanachumbiana.

Kwenye Video hiyo Oprah anaonekana akimnyooshea Mdee kidole huku akisema "Usiwe starehe sana mpenzi, hata mimi nilikuwa kila kitu kwake"

Wanamitandao wengi hata hivyo hawajaridhishwa na kitendo cha Oprah huku wengi wakimwambia akubali hali ilivyo na asonge mbele na maisha yake.

Siku ya Jumatano Mdee na Rotimi walitangaza kuwa wanatarajia mtoto wao wa kwanza hivi karibuni.





Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz