Uwoya Atawatoa Roho Watoto wa Watu - EDUSPORTSTZ

Latest

Uwoya Atawatoa Roho Watoto wa Watu
HABARI ikufikie kwamba, supastaa wa Bongo Movies mwenye maisha yake Bongo, Irene Uwoya ipo siku atawatoa watoto wa watu roho mjini.

 

Hii ni baada ya kuonekana akiringishia simu yake mpya aina ya Iphone 13 Pro Max almaarufu macho matatu, kiasi cha kusababisha gumzo kama lote.

 

Uwoya ameposti video akiringishia simu hiyo mpya wakati akiitoa kwenye maganda yake huku ikisikika sauti ya ‘chawa wake’, Aristote akisema kuwa, mwanamama huyo hatumii nguvu kuifungua simu hiyo mpya halafu ataitumia hivyohivyo bila kava kuonesha jeuri ya pesa aliyonayo.

 

IJUMAA WIKIENDA limeelezwa kuwa, simu hiyo ndiyo inayowatoa watu roho mjini ambapo miongoni mwa stori zinazosambaa mitandaoni, yumo mrembo aliyediriki kuuza figo yake ili amililiki simu hiyo.

 

Uchunguzi wetu umebaini kwamba, simu hiyo ambayo nit oleo jipya kutoka Kampuni ya Apple, kwa nchini Tanzania inapatikana kwa bei ya shilingi milioni nne na laki moja (4,100,000/=).

 

Miongoni mwa sifa za simu hiyo ni pamoja na uzito wa gram 240, inaingia chaji fasta na kwa njia ya wireless, ina rangi za dhahabu, bluu na silva, saizi ya kiooo ni inchi 6.70, ni touch screen, ina resolution ya pixels 1284×2778, storage ya GB 128, kamera moja matata ya nyuma na mbele, inapokea Wi-Fi popote, GPS, Bluetooth na makorokoro mengine yote unayoyajua kwenye simu.

 

Uwoya anatajwa kuwa ndiye staa wa Kibongo anayeongoza kwa kuishi maisha ya kifahari zaidi kuliko staa mwingine yeyote.


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz