Utajiri wa Harmonize, Rayvanny ni Balaa Tupu - EDUSPORTSTZ

Latest

Utajiri wa Harmonize, Rayvanny ni Balaa Tupu


HATA wewe ukiulizwa kati ya msanii Rayvanny kutoka Lebo ya WCB na Haromonize, bosi wa Konde Gang nani ana mkwanja mrefu? Utaweweseka.

 

Kwanza; kwa sababu mali wanazomiliki mastaa hao wa muziki wa vijana Bongo, haziko kwenye rekodi zilizo wazi. Lakini pili, miruzi ya watu itakupoteza.

 

Wapo wanaoamini kuwa, Rayvanny amemzidi sana Harmonize kimapato kutokana na kile kinachotajwa kuwa, anapiga mkwanja mrefu kupitia mitandao ya kijamii inayodili na muziki.

 

Kwa mfano, hivi karibuni takwimu za mtandao wa Spotify zinaonesha kuwa, Albam ya Rayvanny ya The Sound From Africa, imetazamwa na watu 24Mil, huku ile ya Harmonize iitwayo AfroEast ikiwa imewavutia watu 1.2Mil.

 

Unapozungumzia watazamaji kwenye mitandao kama BoomPlay, YouTube, Spotify na mingineyo unakuwa unazungumzia fedha kwani kadiri unavyotazamwa na wengi ndivyo unavyolipwa kikubwa.

 

Lakini kwa upande mwingine kuna watu wanasema, Harmonize anamzidi mtonyo Rayvanny kwa sababu kwanza, kipato chake hakimegwi na pande nyingi kwa vile msanii huyo ana Lebo yake.

 

Kingine Harmonize anaingiza fedha nyingi kupitia balozi za makampuni anazopata tofauti na Rayvanny ambaye anatajwa kuwa hayupo vizuri kwenye engo hiyo.

 

Yote kwa yote ni kwamba, Harmonize anapata “bichwa” la kuwa na faranga nyingi kwa sababu ni mtu anayejitegemea na kwamba kazi anazofanya mapato yake hayagawanywi kwenye Lebo kama anavyofanyiwa Rayvanny ambaye mpaka sasa ameshindwa kujichomoa WCB ili afanye kazi zake binafsi.

 

Hivi karibuni Rayvanny alitangaza kuanzisha Lebo yake iitwayo Next Level lakini taarifa za chini ya kapeti zinasema, amekwama kulipa fedha kama kikomboleo cha kutoka WCB ambayo imetajwa kufikia 1.5Bil.

 

Harmonize alipotaka kuondoka WCB na kuanza kujitegemea aliambiwa atoke 500Mil kama kikomboleo ambazo alitoa na kuwa huru kimuziki na kimapato. Kwa hoja hii wewe mwenyewe unaweza kujiongeza na kupata jibu nani kati ya Harmonize na Rayvanny ana kufuru ya fedha?


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

1 comment:

Edusportstz