Steve Nyerere Amchamba Ney wa Mitego Achana Kuimba Uharakati Upate Hela" - EDUSPORTSTZ

Latest

Steve Nyerere Amchamba Ney wa Mitego Achana Kuimba Uharakati Upate Hela"


Steve Nyerere anamsikitikia msanii #Naytrueboy kwa kung'ang'ania kuimba nyimbo za kiharakati ambazo hazimuingizii kipato wala hazimfanyi aitwe kwe show zaidi ya kupata sifa Twitter na Instagram wakati angeweza kuimba nyimbo za kumuingizia kipato badala ya kuambulia sifa tu

Reposted from @stevenyerere2 Kwa Nyimbo nzuri Mashairi yako Mazuri na haukuanza Leo  kitambo sana na  kizuri zaidi  Unasimama na unacho kiamini ni jambo zuri sana, Hakuna Binadamu anaweza kumpangia Binadamu mwenzio nini cha kufanya lakini kama unampenda na kumkubali Unaweza kumshauri kwa Faida yake ya kesho na kesho kutwa,  Mimi ushauri wangu  Kwa kipaji Alicho kupa Mungu ungeweza kufanya Nyimbo za kukuingizia hela  na kukufanya ukaitwa kwenye shoo mbali mbali nadhani ungetusua sana,  Maana una uwezo mkubwa sana wa kuimba ni Muda sasa ungeimba Mashairi Ambayo kila kona, kila Bar, kila mtaa  unasikia Nyimbo mpya kutoka kwa Ney, Ukiingia Disko zote ni shida kuliko hizi nyimbo za harakati Ambazo Faida yake ni matatizo na watu, Lakini nikifika mbali kabisa Naimani Umri wako unahitaji FEDHA ili kufanikisha malengo yako kama kijana kufikia ndoto zako, Hukatazwi kuwa mwanaharakati lakini mwanaharakati mzuri ni yule ambaye amesha jidhatiti kwa kesho yake kuto kuyumba hata kitokee kitu chochote, Africa wanaharakati sio wengi hivo lakini Ukiwatafuta kwa Taifa kama letu hatuna wana harakati wa kweli wengi waganga njaaa na wengine wanaweza kutumia watu kwa Faida zao binafsi, Natambua Taifa letu limewajengea wananchi wake Uhuru wa kusema lakini kumbuka baada ya kusema,  Ndugu yangu NEY  RUDI kwenye zile Nyimbo zako zilizokufanya uwe Ney na kukuingizia kipato na shoo za kumwaga, Zilizokufanya kila kona na Radio wanapiga nyimbo zako, Shoo zote ukawepo na kujipatia kipato chako,Achana na hizi nyimbo za Twitter  na Instagram  Pongezi nyingi na wanasiasa lakini ukiangalia pongezi za nyimbo na kipato ulicho ingiza kupitia nyimbo ni vitu 2 tofauti,  Bado naimani na wewe sana sana na natambua una uwezo mkubwa na mchango mkubwa kwenye sanaa ya Tanzania basi ni Muda sasa wakuungana na Serikali ya Awamu ya 6 kupaza sauti ya maendeleo na sio kebehi,  Natambua Kipaji chako, Lakini kwa nyimbo hizi kwa nchi zetu za Africa kukuingizia kipato bado sana sana, Ni ushauri wangu tu kama unaweza kustuka stuka njoo tujenge Taifa kwa umoja na mshikamano wetu, Natamani ukapiga manyimbo  kama wanayopiga wenzako maana uwezo uo unao tena mkubwa sana na kipaji hicho cha kusikilizwa unacho kinashindikana nini kuingiza kwanja,  

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz