Senzo Aichimba Mkwara Mzito Simba - EDUSPORTSTZ

Latest

Senzo Aichimba Mkwara Mzito Simba




BAADA ya kutangazwa kuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Yanga, Senzo Mazingiza amechimba mkwara mzito kuwa ni lazima kikosi hicho kifanye makubwa, na kukamilisha malengo ambayo wamejiwekea ikiwemo kutwaa ubingwa ulio kwa Simba.

 

Senzo alitangazwa rasmi kushika wadhifa huo ndani ya Yanga kwa lengo la kuhakikisha anakamilisha mchakato wa mabadiliko ya kiuendeshaji kama ambavyo iliazimiwa na Wanachama wa klabu hiyo katika mkutano mkuu uliofanyika Juni 27, mwaka huu.

 

Kabla ya majukumu hayo kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita tangu amejiunga na Yanga, Senzo alikuwa akihudumu kama mshauri mkuu wa mabadiliko.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Senzo alisema: “Tumefanya usajili mzuri katika dirisha la usajili lililopita, lakini tumekuwa na mipango bora kuelekea msimu ujao kama uongozi kuhakikisha tunafikia malengo ambayo tumejiwekea.

 

“Kwangu nikuhakikishie kuwa nina matumaini makubwa ya kukamilisha malengo ambayo tumejiwekea na kurejesha furaha kwa Wanayanga.”

JOEL THOMAS




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz