Samuel Eto Atangaza Kugombea urais wa Shirikisho la Soka Cameroon - EDUSPORTSTZ

Latest

Samuel Eto Atangaza Kugombea urais wa Shirikisho la Soka CameroonNyota wa mpira wa soka nchini Cameroon Samuel Eto atangaza kugombea urais wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Cameroon.

Tangazo hilo limetolewa Jumanne katika ukurasa wake rasmi wa Facebook.

"Nimeamua kuchukua uamuzi huu kwasababu ya kuipenda Cameroon na kupenda soka yetu", alielezea Samuel Eto katika taarifa yake.

Aliandika pia, "ni wakati wa kujenga upya mpira wetu".

Baada ya uvumi kadhaa, Samuel ameamua kuwa mgombea wakati kuna utata juu ya marufuku ya uraia mara mbili nchini Cameroon.

Samuel Eto alikuwa raia wa Uhispania wakati alikuwa akicheza Uhispania.

Miongoni mwa masharti yanayotakiwa kuwa mgombea wa urais wa shirikisho la mpira wa miguu la Cameroon, ni marufuku ya kuwa na utaifa wa kigeni.

Samuel Eto ni kigogo wa tatu wa zamani kugombea urais wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Cameroon.

Hata hivyo, bado haijulikani ikiwa ugombea wake utathibitishwa.

Uchaguzi umepangwa kufanyika Desemba 11.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz