WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega ameeleza sababu ya nyama kupanda kwa bei katika maeneo mbalimbali nchini ni kutokana na upungufu wa upatikanaji wa ng’ombe na ongezeko la mahitaji ya viwanda vya kuchakata nyama.
“Taarifa ya kupanda kwa bei ninayo, tayari wizara imeshatoa maelekezo ya nini kifanyike. Lakini hata hivyo hii ni dalili njema kwa wafugaji sasa wanahitaji kuwekeza zaidi katika ufugaji,” amesema Ulega.
Hata hivyo wafanyabiashara wa mifugo na wauza mabucha wamesema kuwa kupanda kwa kitoweo hicho kuanzia wanakochukua (machinjioni), gharama za usafirishaji na msimu huu wa kiangazi kumesababisha pia bei ya nyama kupanda kwani wafugaji wengi hawapendi kuuza ng’ombe wakati huu wakidai kwamba mifugo hiyo inakua haina uzito kutokana na kupungua kwa malisho na maji.
Bei ya nyama kwenye mikoa ya Arusha, Moshi na Dar es Salaam inadaiwa kuwa shilingi 7,000 mpaka shilingi 8,000 kwa kilo tofauti na awali ambapo kitoweo hicho kilikua kikiuzwa shilingi 6,000
Post a Comment