Promota PCK Afunguka Ukweli Mchungu "Harmonize Mdogo Sana Huwezi Fanya Nae Show Marekani Ikalipa" - EDUSPORTSTZ

Latest

Promota PCK Afunguka Ukweli Mchungu "Harmonize Mdogo Sana Huwezi Fanya Nae Show Marekani Ikalipa"


Moja ya Promota mkubwa sana kwa sasa hapa Bongo na anayeanda shows za wasanii ndani na kimataifa yani nje ya nchi Pck amedai kuwa msanii kutoka KondeGang Harmonize bado ni msanii chipukizi nchini Marekani.

Akitoa ufafanuzi kuhusu gharama za shows za wasanii wa Africa wanaokwenda kufanya kazi marekani katika kipindi cha Leo Tena ya clouds FM.

PcK amemtaja msanii harmonize kama msanii mdogo/chipukizi kwa kwenda kufanya show marekani akieleza kuwa pia ni mara yake ya kwanza kwa msanii huyo kwenda nchini humo kufanya show.

Hivyo bado ana kazi kubwa ya kupambana ili kufikia ukubwa wa wasanii kama Davido, Burnaboy Diamond Tekno, Yemialade Tiwasavage na Wizkidayo ambao hao wanauwezo wa kufanya show Marekani na pesa ikarudi ila si kwa Harmonize kwa sababu unaweza weka pesa yako ukapata hasara tu.

Nini maoni yako πŸ‘‡

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz